Mkusanyiko: Drones za Kirusi

Kampuni kubwa zaidi duniani ya kutengeneza ndege zisizo na rubani DJI imesitisha shughuli zote za biashara nchini Urusi na Ukraine.

Tangu kuanza kwa vita hivyo, Ukraine imeitaka kampuni hiyo kuchukua hatua kukomesha ndege zake zisizo na rubani kutumiwa na Urusi.

Kampuni hiyo ya China ilisema uamuzi huo sio taarifa kuhusu nchi yoyote, na ndege zake zisizo na rubani si za matumizi ya kijeshi.

Lakini Taras Troiak, mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa UAV wa Ukraine, aliiambia BBC kuwa ana shaka kuwa ingesimamisha jeshi la Urusi kutumia ndege zisizo na rubani za DJI.

Alisema kuwa vifaa vya madukani vya ndege zisizo na rubani vinaweza kuisha katika miezi michache lakini, kwa maoni yake, vinaweza kuingizwa nchini Urusi kwa urahisi kutoka Uchina.

Ndege hizo zisizo na rubani zinatumiwa na jeshi la Urusi kwa upelelezi wa masafa mafupi, anasema. Kwa maoni ya Bw Troiak hutumiwa "kutazama huku na huko, kutafuta askari wowote karibu na kuhakikisha kuwa hakuna mtu aliye karibu nawe".